Klabu ya Barcelona ya nchini Hispania leo imebadili jina la uwanja wake wa mazoezi na kuupa jina la kocha wa zamani wa klabu hiyo Tito Vilanova aliyefariki Aprili mwaka jana kwa ugonjwa wa kansa ya koo.
Uwanja huo uliokuwa unafahamika kwa jina la Joan Gamper umepewa jina hilo ikiwa ni sehemu ya kumuenzi kocha huyo aliyeifundisha timu hiyo msimu wa 2012/2013.
Zoezi hilo la uzinduzi limefanyika leo asubuhi likuhudhiliwa na wachezaji na viongozi mbalimbali wa timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment