Sporty Magazine official website | Members area : Register | Sign in

Kingine usichokijua kuhusu maisha ya David Beckham…

Monday, 23 March 2015

Share this history on :

becham

Mara nyingi mastaa mbalimbali wamekuwa wakiishi maisha ya kuwafanya waonekana vyema mbele ya mashabiki wao na hata wengine kuishi maisha ambayo si yao ili mradi wawe kivutio kwa mashabiki wao.

Hilo limekuwa tofauti kidogo kwa mkongwe wa soka duniani David Beckham ambaye pia ni mwanamitindo baada ya kusema amekuwa akimtegemea mke wake Victoria kwa asilimia tisini na tisa katika uvaaji wake.
victoria
Beckam ambaye ni baba wa watoto watatu pia amesema yeye mara zote amekua akivutiwa na uhalisia wa maisha ya watoto wake ambao wamekuwa wakimvutia kwa kiasi kikubwa.
NY Fashion Week Victoria BeckhamMchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid alisema pia huwa anavutiwa sana na staili ya watoto wake kuanzia mavazi na jinsi wanavyoishi,huku akimtolea mfano mtoto wake wa kwanza Brooklyn ambye amekiri kuwa amekuwa na mwonekano wa peke yake ambao humvutia wakati wote.
Mbali na Brooklyn amesema pia watoto wake wengine Romeo pamoja na Cruz nao  wamekuwa wakimvutia wakati wote.
Thank you for visited me, Have a question ? Contact on : youremail@gmail.com.
Please leave your comment below. Thank you and hope you enjoyed...

0 comments:

Post a Comment