Jose Mourinho hakukubalina na maamuzi ya mwamuzi kumtoa nje kwa kadi nyekundu mlinzi na nahodha wa Chelsea John Terry kwenye mechi ya jana wakati Chelsea ilipocheza dhidi ya West Brom mchezo wa ligi kuu England, lakini Mourinho amesema kukata rufaa ni kupoteza muda.
Terry alitolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi Mark Clatternburg kipindi cha pili kufuatia kumfanyia madhambi Salomon Rondon wakati Chelsea ilipopata ushindi wa kwanza msimu huu kwenye EPL kwa kuifunga West Brom kwa goli 3-2.
“Kukata rufaa ni sawa na kupoteza muda”, Mourinho aliwaambia waandishi
“Nadhani tunatakiwa kukata rufaa, lakini ni kupoteza muda, Nemanja Matic dhidi ya Burnley msimu uliopita ilikuwa ni kupoteza muda, Thiago Silva dhidi ya Liverpool ilikuwa ni kupoteza muda”
Courtois alioneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo ambao Chelsea ililazimishwa sare ya goli 2-2 ikiwa nyumbani dhidi ya Swansea City na Mourinho akasema alikuwa ameiandaa timu yake kucheza ikiwa na wachezaji 10.
Mourinho aliongeza: “Nalazimika kufundisha wachezaji 10 dhidi ya 11. Tulifanya hivyo mara kadhaa tukiwa Canada, na tunahitaji kuendelea kufanya hivyo.
Tunatakiwa kujua cha kufanya pale timu inapobakiwa na wachezaji 10 unapokuwa umeshinda, wachezaji 10 unapokuwa umefungwa, wachezaji 10 unapokuwa unahitaji matokeo, wachezaji 10 unapokuwa unalinda ushindi na tofauti kati ya jana na mchezo dhidi ya Swansea ndiyo ilikuwa hiyo.
Dhidi ya Swansea timu ilikuwa na wachezaji 10 ikihitaji kubadilisha matokeo wakati jana tulikuwa 10 na tunahitaji kulinda matokeo.
0 comments:
Post a Comment