Sporty Magazine official website | Members area : Register | Sign in

Podolski atamani kurudi Arsenal

Thursday, 12 March 2015

Share this history on :

Internazionale Milano vs AC FiorentinaNa Augustino Mabalwe,Dar es salaam
Baada ya Lukas Podolski kushindwa kuonesha makali yake katika klabu ya Intermilan huko nchini Italia,mshambuliaji huyo amesema anataka kurejea katika klabu ya Arsenal ili aweze kuonesha uwezo wake baada ya hapo mwanzo kushindwa kung’ara.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani amejiunga na Intermilan kwa mkopo katika kipindi cha dirisha dogo mwezi januari mwaka huu baada ya kushindwa kuonesha makali yake ya zamani katika klabu ya Arsenal.
Podolski,29, amekuwa na wakati mgumu tangu ajiunge na wababe hao wa zamani wa italia na mpaka sasa hajafanikiwa kufunga hata goli moja,hivyo ameona bora kurejea katika timu yake ya Arsenal.
“Nimebakiza mkataba wa mwaka mmoja katika klabu ya Arsenal hivyo nikirejea na nikapewa nafasi nitaweza kuonesha uwezo wangu ili niwaridhishe mashabiki kwani bado wananidai ” alisema Podolski.
Mshindi huyo wa kombe la dunia mwaka 2014 amesema atajitahidi kutumia uwezo wake ili kuisadia timu hiyo ya Robarto Mancin inayoshika nafasi ya 9 katika ligi kuu nchini Italia.
Thank you for visited me, Have a question ? Contact on : youremail@gmail.com.
Please leave your comment below. Thank you and hope you enjoyed...

0 comments:

Post a Comment